Azam fc yatinga Fainali
Klabu ya soka ya Azam fc imefanikiwa kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho (FA CUP) baada ya kuibwaga Mwadui FC kwa Penati 5-3
Penalti hizo zilipigwa baada ya Sare ya 2-2 katika Dakika 120 za Mchezo.Azam FC walitangulia kuifunga Mwadui FC kwa Bao la Dakika ya 3 la Mcha na Mwadui FC kusawazisha Dakika ya 82 kupitia Kabunda.
Mechi ikaenda Dakika za Nyongeza 30 na kila Timu kufunga Bao 1 zaidi kwa Mcha kuipa Azam Bao la Pili Dakika ya 97 na Mwadui kusawazisha kwa Penati ya Dakika ya 123 kwa Bao la Aziz.
Mechi kati ya Coastal Union na Yanga imevunjika baada ya kuchezwa Dakika 15 tu za Dakika za Nyongeza 30 huku Yanga wakiongoza 2-1.
Mechi ya Yanga vs Tanga Coastal imevunjika kutokana na vurugu za Mashabiki huku pia giza likishamiri Uwanjani.
Huko Mkwakwani Tanga Coastal walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 55 la Yusu Sabo na Donald Ngoma kuisawazishia Yanga katika Dakika ya 61.
Bao hizo zilibaki hadi Dakika 90 zinakwisha na kuongezwa Dakika za Nyongeza 30 na yanga kufanikiwa kuandika Bao lao la Pili Dakika ya 95 Mfungaji akiwa Amisi Tambwe.
Dakika ya 101, Coastal walibaki Mtu 10 baada ya Adeyum Ahmed kupewa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Hadi Dakika 15 za kwanza kumalizika, Yanga walikuwa mbele kwa Bao 2-1 lakini Mechi hii ikavunjika kutokana na vurugu za Mashabiki huku pia giza likishamiri Uwanjani.
Hivyo ripoti ya kutoka kwa kamisaa wa mchezo pamoja na kamati ya mashindano itatoa majibu sahii kuhusiana na mchezo huo.
http://www.bbc.com/swahili/michezo/2016/04/160425_azam_fainali
Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP
Klabu ya soka ya crystal Palace
imetinga hatua ya Fainali ya FA CUP baada ya kuifunga Watford United Bao
2-1 kwenye Nusu Fainali.
Kwa matokeo hayo ya mchezo huo
uliochezwa Uwanjani Wembley, Jijini London, sasa Palace watakutana na
Manchester United ambao waliwatoa Everton 2-1 katika Nusu Fainali
nyingine.Hadi Mapumziko Palace walikuwa mbele kwa Bao 1-0 lililofungwa na Yannick Bolasie.
Kipindi cha Pili, Watford walimudu kusawazisha kupitia Deeney lakini Dakika 6 tu baadae Connor Wickham akafunga Bao la Pili na la ushindi kwa Palace.
Fainali Michuano hii itachezwa Mei 21 hapo hapo katika dimba laaWembley.
Esperance yaizamisha Azam!!
Klabu ya soka ya Azam FC imeaga
michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika baada ya kufungwa mabao
3-0 na wenyeji Esperance katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora
kwenye mechi iliyoandaliwa mjiniTunis, Tunisia.
Matokeo hayo
yanafanya Azam FC inayomilikiwa na bilionea Alhaj Sheikh Said Salim
Awadh Bakhresa na familia yake, itolewe kwa jumla ya mabao 4-2, baada ya
awali kushinda 2-1 mjini Dar es Salaam.Mabao ya Esperance yalifungwa na wachezaji Saad Bguir dakika ya 47 kwa shuti la mpira wa adhabu umbali wa mita 19, Dakika ya 63.
Haithem Jouini alifunga kwa kichwa akimalizia mpira uliotemwa na kipa Aishi Manula kufuatia krosi ya Hoiucine Regued na dakika ya 80, Fakhreddine Ben Youssef akafunga la tatu akimalizia pasi ya kiungo Driss Mhirsi.
Serengeti Boys kujipima na nchi nne
Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana
wenye umri chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' inatarajiwa kushiriki
mashindano maalumu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini India,
yatakayozishirikisha nchi za Marekani, Malasyia na Korea Kusini na
wenyeji mapema mwezi Mei, 2016.
Chama cha Soka nchini India (AIFF)
kimeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la
Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.Jumla ya nchi tano zitashiriki mashindano hayo yatakayofanyika katika mji wa Goa kuanzia Mei 15-25, 2016 ambapo michezo itachezwa kwa mfumo wa ligi kwa kila timu kucheza michezo minne, kabla ya mchezo wa mwisho wa fainali wa kumpata Bingwa wa mashindano hayo.
Serengeti Boys ambayo imeshacheza michezo mitatu ya kirafiki ya kimataifa mpaka sasa, mmoja dhidi ya Burundi na miwili dhidi ya timu ya vijana wa Misri (The Pharaohs) inatarajiwa kuingia kambini mwishoni mwa mwezi Aprili, 2016 katika hosteli za TFF zilizopo Karume kujiandaa kwa safari ya kuelekea nchini India kushiriki michuano hiyo.
Kikosi cha Serengeti Boys kinachonolewa na kocha Bakari Shime, akisaidiwa na Sebastian Mkomwa chini ya mshauri wa ufundi wa timu za vijana Kim Poulsen, kinatarajiwa kuwa kambini kwa muda wa wiki mbili kabla ya safari kuelekea Goa India kushiriki mashindano hayo.
Kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo maalumu ya vijana kimataifa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Serengeti Boys, kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za vijana barani Afrika dhidi ya Shelisheli Juni 25 hadi Julai 2, 2016.
0 comments:
Post a Comment