VICHWA VYA HABARI

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks t>

Friday, April 15, 2016

Wawekezaji wa madini Tanzania wataka kujadili na serikali yao jinsi ya kuboresha mazingira ya biashara hiyo


kutoka mataba katoro fm
madini hali ambayo itawatorosha wawekezaji wa kigeni. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya maofisa wa migodi ya madini nchini humo wamesema kuna changamoto kadhaa ambazo zimechangia wawekezaji katika sekta ya madini kutowekeza kwenye utafutaji wa madini jambo ambalo linaweza kuifanya sekta hiyo kuporomoka au kudumaa.
Mwenyekiti wa Chama cha Madini na Nishati Tanzania Bw Ami Mpungwe amesema kuna haja kubwa ya serikali kukutana na wawekezaji wa madini kwa sababu kuna tabia ya kushutumiana na kulaumiana kila upande jambo ambalo linaweza kutatuliwa kwa mazungumzo. Mpungwe amesema mkutano huo ulikuwa muhimu kwa faida ya wawekezaji na serikali. Ameongeza kuwa wadau kwenye sekta ya madini wana kilio kikubwa ambacho suluhisho la uwekezaji wa sekta hiyo ni serikali kukaa na wawekezaji na kusikia malalamiko yao.
http://swahili.cri.cn/141/2016/04/15/1s152591.htm 

0 comments:

Post a Comment