VICHWA VYA HABARI

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks t>

Thursday, March 17, 2016

TAMISEMI YAAGIZWA KUSIMAMIA VIZURI MIKOA NA HALMSHAURI ILI KULETA MAENDELEO TARAJIWA.

Waziri Mkuu Aagiza OR TAMISEMI Kusimamia Mikoa na Halmashauri Kuleta Maendeleo tarajiwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameitaka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-(OR-TAMISEMI) kuhakikisha inaisimamia vizuri Mikoa na Halmashauri ili serikali iweze kupata matokeo mazuri na tarajiwa.Akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI alipoitembelea ofisi ya TAMISEMI mjini Dodoma leo, Mhe. Waziri Mkuu alisema jukumu kubwa lililopo hivi sasa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ni kuhakikisha kuwa zinabuni vyanzo vipya vya mapato na kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato ya serikali.
“Hatukubaliani na uzembe kwenye idara na halmashauri za wilaya kwakuwa hivi sasa serikali ya awamu ya tano inasimamia utumishi wa uadilifu hivyo kila mmoja ahakikishe anasimamia vizuri eneo lake” alisema Mhe. MajaliwaAlisema serikali ya awamu ya tano imekusudia kuwahudumia ipasavyo watanzania wenye uelewa tofauti na matakwa tofauti na kwa kuanzia serikali imeanza kuwajenga watumishi wa serikali kutambua na kukumbuka kuwa wao ni wahudumu wa wananchi hivyo inawapasa kuwahudumia vema.
“Lazima tujenge moyo wa huruma wa kuwahudumia wenzetu, anapokuja mwananchi msikilize, muhudumie na mwelekeze eneo sahihi ili aweze kupata huduma. Lazima tusimamie na kuona maeneo yote yanafanya kazi kama ilivyokusudiwa, ili kupata matokeo tarajiwa iwe ni wajibu ya kila mmoja kuhakikisha kuwa anatoa usimamizi thabiti katika eneo lake.” alisisitiza Mhe. Waziri Mkuu.
Akimkaribisha Mhe. Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene alisema TAMISEMI wapo tayari kubadilika na kufanya kazi kama kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli –HAPA KAZI TU-.

http://www.pmoralg.go.tz/newseventsinfo/habari-1100-20160121-Waziri-Mkuu-Aagiza-OR-TAMISEMI-Kusimamia-Mikoa-na-Halmashauri-Kuleta-Maendeleo-tarajiwa/ 

Naibu Waziri apiga marufuku eneo la Shule kutumika kibiashara


Naibu Waziri apiga marufuku eneo la Shule kutumika kibiashara
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo, ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, kufuta mawazo ya kubadilisha matumizi Shule ya Msingi Uhuru Wasichana kama eneo la kibiashara.
Aidha amemtaka Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Isaya Mngurumi, kutoa kipaumbele kwenye malipo ya fedha za likizo na kupandishwa daraja kwa walimu wa shule hiyo, kutokana na kufanya kazi kwenye mazingira magumu.
Pia amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa kuhakikisha kuwa Shule hiyo haikosi karatasi maalum za kuchapishia maandishi ya nukta nundu, kwa wanafunzi wasioona.
Naibu Waziri alitoa maagizo hayo Dar es Salaam, tarehe 17 februari 2016 wakati alipotembelea shule hiyo ili kufahamu changamoto mbalimbali zilizopo.
Alisema lazima maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ya kutaka Shule ya Uhuru wasichana isibadirishwe na kutumika kwa matumizi ya kibiashara yatekelezwe.
Mheshimiwa Jafo aliitaka halmashauri hiyo kuboresha miundombinu ya shule ili iendelee kutoa elimu kwa watoto kwa sababu bado serikali inahitaji uwepo wa shule za kutosha.
“Kama bado mna mawazo ya kubadirisha matumizi ya shule ya Uhuru wasichana ni bora muyafute, nataka maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu, yatekelezwe” alisisitiza.
Mheshimiwa Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, alionyesha kusikitishwa na mazingira magumu wanayokabiliana nayo walimu wa shule ya Uhuru mchanganyiko, ambao wanafundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Kutokana na hali hiyo, Naibu Waziri alimuagiza Mkurugenzi na Ofisa Elimu wa halmashauri hiyo, kuongeza magodoro yanayotumiwa na wanafunzi hao kufanyia mazoezi.
Aliongeza kuwa, walimu wa shule hiyo wanapaswa kupewa kipaumbele kwenye malipo ya likizo pamoja na kupandishwa madaraja kutokana na kufanyakazi kwa moyo wa kujituma.
“Mkurugenzi sitaki kusikia malalamiko kuhusu kucheleweshwa malipo ya likizo au kupandishwa madaraja kwa walimu hawa.
“Wamekuwa wakifanya kazi kwenye mazingira magumu lakini kwa moyo wa kujitolea hivyo nataka wawe wanapewa kipaumbele zaidi kwenye maslahi yao” alisema.
Naibu Waziri alisema, serikali itatilia mkazo upatikanaji wa vifaa maalum vya kufundishia ili wanafunzi wenye mahitaji maalum waweze kusoma bila vikwazo vyovyote.
Aliwataka wazazi walio na watoto wenye ulemavu, kutowaficha majumbani bali wawapeleke shuleni kupata taaluma.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana, alimpongeza Waziri Jafo kwa kufika kujionea changamoto zilizopo ili ziweze kufanyiwa kazi.
Alisema, wanafunzi wenye mahitaji maalum wanahitaji uwepo wa vifaa vya kutosha vya kujifunzia.
Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1921, ina wanafunzi 64 wasioona, 22 viziwi pamoja na upofu, 79 wenye mtindio wa ubongo pamoja na wanafunzi watano wenye ulemavu wa ngozi. 

Kashfa ya rushwa: FIFA yawageukia viongozi wa zamani


Gianni Infantino, Rais mpya wa FIFA. Ijumaa Februari 26, 2016 mjini Zurich.
Gianni Infantino, Rais mpya wa FIFA. Ijumaa Februari 26, 2016 mjini Zurich.
FIFA TV

Na RFI
Enzi mpya yafunguliwa katika Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA), ambapo rais mpya aliyechaguliwa, Gianni Infantino, ameahidi kurejesha picha na sifa nzuri kwa FIFA kwa kupambana kwa hali na mali dhidi ya rushwa. FIFA imewataka baadhi ya viongozi wa zamani wa shirikisho hilo kujieleza.

Wiki mbili baada ya uchaguzi wa Gianni Infantino, Shirikisho la Soka Duniani limeanza kubadili mkakati katika kesi inayojulikana kama "Fifagate". Baada ya kulaumiwa na mahakama ya Marekani kwa karibu mwaka mmoja kwa ufisadi mkubwa, Shirikisho la kimataifa la Soka linaonekana kuwa limeathirika kutokana na viongozi walioza kwa rushwa ambao walitumia vibaya nafasi zao kwa kujihusisha na fedha badala ya soka.
Katika taarifa iliyotolewa Jumatano hii, Machi 16, FIFA imetangaza kwamba imeomba fidia kwa watu 41, wengi wao wakiwa maafisa wa zamani wa FIFA, na ambao kwa sasa wanatuhumiwa na mahakama ya Marekani. Kwa hivyo, Shirikisho la Soka Duniani limeomba Mwendesha Mashitaka Mkuu wa jimbo la New York kushughulikia madai yake, kama taasisi iliyofanyiwa unyonge.
Afrika Kusini yashutumiwa kununuwa michuano ya Kombe la Dunia
FIFA inataka sio tu kurejeshewa fedha ziliopitishwa mlango wa nyuma na washitakiwa, lakini pia katika kurejeshewa mishahara, marupurupu na mafao mengine ambayo walilipwa wakati wa shughuli zao katika Shirikisho. FIFA inabaini kwamba fedha hizo zinakadiriwa kufikia mamia angalau ya mamilioni ya Euro, ambapo rais mpya kuzitumia katika maendeleo ya mpira wa miguu.
Watu wanaolengwa wanatoka katika bara la Amerika. Lakini pia Afrika Kusini, ambayo inashutumiwa kutoa dola milioni kumi kama rushwa ili kuhakikisha inaandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 katika ardhi yake.
tags: Shirikisho la Soka Duniani FIFA - Gianni Infantino - Afrika Kusini
 
  http://www.kiswahili.rfi.fr/afrika/20160316-kashfa-ya-rushwa-fifa-yawageukia-viongozi-wa-zamani

Vijana wandelea kutowakilishwa katika mabunge duniani : Ripoti

Nembo ya IPU.(Picha@IPU)
Ripoti mpya ya muungano wa mabunge duniani IPU inaonyesha kuendelea kwa tatizo sugu la kutowakilishwa ipasavyo kwa vijana katika mabunge, wakati huu ambapo idadi ya kundi hilo duniani ni ikubwa kuliko wakati wowote ule.
Ripoti hiyo iitwayo uwakilishi wa vijana katika mabunge ya kitaifa 2016, iliyozinduliwa leo wakati wa mkutano kuhusu wabunge vijana unaofanyika mjini Lusaka Zambia, imeabaini kwamba ni asilimia 1.9 pekee kati ya wabunge 45,000 wana umri chini ya miaka 30.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa hakuan ongezeko kutokana na utafiti wa IPU wa mwaka 2014 ambapo pia ripoti imeonyesha kuwa karibu theluthi ya mabunge madogo na karibuasilimai 80 ya mabaraza ya seneti hayana hata mbunge mmoja mwenye umri wa chini ya miaka 30.
Hata hivyo ripoti mpya hiyo imetaja nchi ambazo zimepiga hatua katika kuwajumisha vijana katika mabunge yao kuwa ni Sweden, Ecuador, Finland na Norway ambazo zina asilimia 10 au zaidi ya wabunge wenye umri wa chiniya miaka 30.
Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mjumbe wa vijana katika Umoja wa Mataifa, Ahmad Alhendawi, amesema kuna haja ya kutafuta njia za kuwashirikisha vijana zaidi, hata kutumia teknohama.
(Sauti ya Alhendawi)
"Ningependa kusisitiza umihimu wa kutambua kuwa vijana wanataka kushiriki na wana uwezo wa kushiriki, na tusiwalaumu tu bila kujua ni kwa nini hawashiriki, kwa sababu wakati mwingine kuna vizuizi vikubwa vya kimfumo."

http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/2016/03/vijana-wandelea-kutowakilishwa-katika-mabunge-duniani-ripoti/#.VurnflKbkdU 

Tuesday, March 15, 2016

Malawi yachoma pembe za ndovu haramu

Shirika la wanyama pori la Afrika linasema kuwa ndovu takriban elfu 35 waliuwawa barani humo mwaka jana.
Pembe za ndovu haramu zikichomwa.
  Malawi ilichoma pembe za ndovu takriban mia 8 jummatatu kuonyesha nguvu dhidi ya biashara haramu ya wanyama pori. Maafisa wa forodha walikamata pembe hizo mwaka 2013, pale zilipoingizwa kwa magendo nchini Malawi kutoka Tanzania.
Wafanyakazi wa mbuga ya wanyama walichoma moto takriban tani 2.6 za pembe za ndovu katika hifas=dhi ya mbuga ya Mzuzu kaskazini mwa Malawi.
Shehena ya pembe za ndovu ilikadiriwa kugharimu dola millioni 3.
Brighton Kumchedwa ni mkurugenzi wa mbuga za wanyama pori nchini Malawi.
Bw. Kunchedwa anasema kuwa, kile wanachojaribu kuonyesha ni kuwa ulanguzi wa pembe za ndovu hauna thamani kwa sababu kuna sharia ambayo inapiga marufuku biashara ya kimtaiafa ya pemb za ndovu. Kwa hiyo kile tunachosema ni kuwa, acha usafirishaji haramu wa bidhaa za wanyama pori hususan pembe za ndovu.
Pembe hizo za ndovu zilikamatwa mwaka 2013 lakini mahakama kuu ya Mzuzu iliwapatia maafisa ruhusa ya kuchoma pembe hizo mwezi huu. Tanzania awali ilizuia kuchomwa kwa pembe hizo, ikisema inahitaji baadhi ya pembe hizo kama ushahidi kwa wa kesi mahakamani nchini tanzania.
Ndugu wawili raia wa Malawi walikamatwa wakiwa na shehena ya pembe za ndovu. Walitozwa aini ya dola elfu 5 mia 5 kwa usafirishaji haramu wa pembe za ndovu.
Hii ni mara ya kwanza kwa Malawi kuchoma pembe za ndovu walokamata. Hio inakuja kufwatia harakati banarani Afrika juu ya kuendelea kuuwawa kiharamu kwa ndovu.
Idara ya wanyama pori ya Malawi inaeleza kuwa Malawi imepoteza takriban nusu ya idadi ya ndovu walokuwa nao tangu mwaka 1980, hususan kutokana na uwindaji haramu. Taifa hilo limekuwa njiapanda kwa wasafririshaji haramu wa pembe.
Kumchedwa anasema serikali inashughulikia suala hilo sasa.
Kumchedwa anasema, pembe hizi zinatokea Tanzania kwa sababau sharia zetu ni dhaifu sana. Lakini hivi tunavyozungumza, tunatathmini sharia, ili ziwe na adhabu kali.
Biashara ya kimataifa ya pembe za ndovu ilisitishwa mwaka 1989, lakini wataalam wanasema uwindaji haramu wa ndovu umeongezeka ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya pembe za ndovu huko Asia.
Shirika la wanyama pori la Afrika, linasema kuwa ndovu takriban elfu 35 waliuwawa barani Afrika mwaka jana.
http://www.voaswahili.com/content/malawi-ivory/3236898.html

CUF yasema baadhi ya wakazi wa Zanzibar wakimbilia Mombasa

Siku kadhaa kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa marudio huko Zanzibar, Chama cha Wananchi -CUF kimesema baadhi ya wanachama wake huko kisiwani Pemba wameanza kukimbilia maporini wakitafuta uwezekano wa kutoroka kisiwani humo na kukimbilia katika mji wa Mombasa nchini Kenya ili kutafuta hifadhi ya ukimbizi.

Ripoti ya Munir Zakaria wa Zanzibar skikliza katika link hapo chini.
Hatua hii inafuatia madai ya kuwepo kwa taharuki na kamata kamata inayoendelea huko dhidi ya watu wanaodaiwa kuhusika na matukio ya kuchomwa moto kwa baadhi ya nyumba.
Uchaguzi mkuu wa marudio unatokana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana ambao ulisemekana uligubikwa na kasoro.
Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar bwana Mohamed Aboud alisema serikali imejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi wa marudio unafanyika katika mazingira ya Amani na utulivu.
Aidha aliwataka wananchi kuondokana na khofu hasa katika kipindi hiki ambacho askari katika jeshi la wananchi wa Tanzania- JWTZ wanaendelea na mazoezi yao ya kawaida ya kila mwaka huko Zanzibar.

Tanzania yaahirisha uzinduzi wa kituo cha mpakani na Kenya

Rais John Magufuli alippofungua Bunge la 11 la Tanzania.
Kuanzishwa kwa kituo kipya cha mpakani kati ya Kenya na Tanzania huko Lungalunga huenda ikachukua muda kabla marais wa mataifa hayo mawili kuzindua rasmi kituo hicho baada ya Tanzania kuomba muda kukamilisha ujenzi wa kituo hicho kwa upande wao.
Mipangilio ya kituo kimoja cha mpakani kati ya Kenya na Tanzania huko Lungalunga huenda kikachelewa kuanzishwa baada ya Tanzania kuomba muda zaidi kukamilisha upande wao.
Akizungumza na sauti ya Amerika  afisa wa forodha anayesimamia kituo hicho upande wa Kenya Pius Sokoko Kwach amesema kuwa  walipaswa kuanza shughuli za kituo kimoja mwezi huu wa tatu lakini Tanzania inachelewesha mpango huo.
Pius anasema “walituambia wanaweka mitandao yao sisi huku tuko tayari  shuhuli katika kituo cha Kenya cha uhamiaji na forodha zinaendelea , hata upande wetu kitu chao kiko tayari ni wao wamalize kisha watuambie  mara tu wakimaliza waje waianzishe kwani tayari tuko na tarakilishi tumishi zao ni wao waweke yetu upande wa Tanzania”.
Bw. Sokoko Kwach amekariri kuwa   kituo hicho  kitapunguza kucheleweshwa kwa  shughuli za biashara na wasafiri wanaotumia mpaka huo kuenda na kutoka nchini Tanzania.
Pius anaendelea kusema “ maana na umuhimu ni kupunguza  vituo vingi ambavyo vinasababisha  ucheleweshaji  shughuli  hizi za one stop border ni kupunguza ucheleweshaji unaosababishwa na  shughuli za kulipisha ushuru wa bidhaa na kuangalia wasafiri kati ya mpaka wa kenya na Tanzania.
Kampuni za mabasi zinazotumia mpaka wa Kenya na Tanzani kupitia Lungalunga zimekaribisha mipango  hiyo ya kituo kimoja mpakani.
Yusuf Kassim ni msimamizi wa kampuni ya mabasi ya Tahmeed  ya Mombasa - Daressalaam.
Aidha Yusuf ameitaka jumuiya ya Afrika Mashariki pia kufuatilia mbali swala la kadi ya ugonjwa wa manjano ambao unaendeleza rushwa hasa kwa wale ambao hawana kadi hizo wanapoingia ama kutoka Tanzania.
Bashiri Seif Saidi aliye dereva wa malori ya kusafirisha chakula cha msaada cha wakimbizi kutoka Mombasa hadi kituo cha wakimbizi cha Nyarugusu nchini Tanzania anasema bado wanalazimika kusubiri mpakani hata zaidi ya siku mbili kabla kuendelea na safari isipokuwa mpaka wa Rwanda na Tanzania.
Kituo sawia na hicho kinachounganisha kenya na Tanzania eneo la Taveta na Holili kilizinduliwa rasmi tarehe 27 mwezi Februari mwaka 2016 kama njia ya kuleta umoja katika jumuiya ya Afrika Mashariki.

http://www.voaswahili.com/content/article/3235108.html 

Rais Magufuli asema hasara ya mishahara hewa inafikia billioni 2.5 kwa mwezi

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli akitoa hotuba ya kitaifa
Rais wa Tanzania  John Magufuli amewaapisha wakuu wa mikoa aliowateua hivi karibuni nchini humo huku akizungumzia upotevu mkubwa wa mapato ya serikali unaotokana na kuwepo watumishi hewa
Akizungumza mara baada ya kuwaapisha wakuu hao  wa mikoa rais Magufuli amesema tatizo la wafanyakazi hewa limekuwa likigharimu serikali fedha nyingi, ambapo ametolea mfano wa uchunguzi uliofanywa katika mikoa miwili ya Dodoma na singida na kubaini takriban wafanyakazi hewa 202 katika halmashauri 14.
Amesema kutokana na hali hiyo na ikichukuliwa taswira ya nchi nzima, hasara inayokisiwa inayotokana na malipo ya mishahara hewa ya wafanyakazi nchini  Tanzania inafikia shilingi billioni 2.5 kila mwezi  huku serikali ikitumia shilingi bilioni 549 kwa mwezi kwa ajili kulipa watumishi wake hivyo amewataka kuzisimamia vyema halmashauri zao.
Wakuu wa mikoa wote 25 walioapishwa baadaye wamesaini kiapo cha uadilifu kilichosimamiwa na kamishna wa maadili ya viongozi wa umma Salome Kaganda, huku makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  akiwatahadharisha juu ya kusimamia vyema matumizi ya fedha za maendeleo.
Rais Magufuli pia  amewaapisha kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA,  Alphayo Kidata na Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa-Takukuru,  Valentine  Mlowola aliyewathibitisha kazini hivi karibuni baada ya kukaimu kwa muda nafasi hizo.

http://www.voaswahili.com/content/tanzania-mishahara-hewa-magufuli/3238329.html

Sunday, March 13, 2016

Arsenal yavuliwa ubingwa -FA CUP

St George na TP Mazembe nguvu sawa

Wachezaji wa TP Mazembe
Michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika imeendelea jana kwa michezo kadhaa.
Miongoni mwa matokeo ya mechi hizo Enyimba ya Nigeria imeibugiza Vitaloo ya Burundi mabao 5-1, St George ya Ethiopia imetoshana nguvu na TP Mazembe ya Drc Congo bao 2-2, Union Douala ya cameroon imechapwa bao 1-0 na Zamalek ya Misri.
Na katika Michuano ya kombe la shirikisho Klabu ya St Eloi Lupopo ya D R Congo imeifunga Ahli Shendi ya sudani bao 2-1, Al Ittihad ya Libya imeichabanga Medeama ya Ghana bao 1-0, na Nasarawa ya Nigeria imeichapa Costantine ya Algeria bao 1-0.
Michuano hiyo inatarajia kuendelea tena march 18 mwaka huu.

Arsenal yavuliwa ubingwa -FA CUP

Michuano ya FA Iliendelea tena jana kwa mabingwa wake Arsenal kuvuliwa ubingwa baada ya kuchapwa na Watford kwa mabao 2-1.
Mabao ya Watford yalifungwa na Odion Ighalo na Adlene Guedioura huku bao la kufutia machozi la Arsenal likifungwa na Danny Welbeck.
Katika mchezo mwingine Manchester United wakiwa nyumbani walibanwa mbavu na West Ham united kufuatia sare ya bao 1-1.


Goli la West Ham lilifungwa na mchezaji Dimitri Payet dakika ya 68 kipindi cha pili, huku bao la kusawazisha la Manchester United likipachikwa na Anthon Martial Dakika ya 83 kipindi cha pili.

Nyumba za chama cha CCM zachomwa Pemba, Zanzibar

Watu wasiojulikana wamechoma moto nyumba za Chama Cha Mapinduzi kisiwani Pemba huku duru ya pili ya uchaguzi ikitarajiwa Machi 20.
Kamishena wa polisi wa eneo la Pemba Kusini Mohamed Shakani amesema watu hao wamechoma maeneo 11 ya kufanyia mikutano na zahanati moja lakini hakuna aliyejeruhiwa.
Amesema mshukiwa mmoja kwa jina Mohamed Ramadhan Seif amekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Shakani anasema uchunguzi wa mwanzo umeonyesha kuwa waliotekeleza kitendo hicho walinyunyiza petroli kwenye nyumba hizo katika barabara ya Kibirizi pamoja na maeneo ya mikutano ya Kiwani na Mwambe na kuwasha moto.
Waziri kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais Mohamed Aboud Mohamed amezuru maeneo hayo na kuwataka raia kusaidia kuwatambua waliotekeleza uchomaji huo.

http://swahili.cri.cn/141/2016/03/13/1s151664.htm 

Tanzania yajinasibu kuhusu takwimu kwenye ajenda 2030

Dokta Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa  Ofisi
 ya Taifa ya Takwimu Tanzania. Picha: Kiswahili Unit
Mkutano wa 47 wa kamisheni ya takwimu ya Umoja wa Mataifa ukifikia ukingoni leo, Tanzania imesema imeshaandaa mpango wa ufuatiliaji wa masuala ya takwimu kwenye utekelezaji wa ajenda 2030 iliyopitishwa mwaka jana.
Akihojiwa na Idhaa hii kando ya mkutano huo uliopitisha viashiria vya kitakwimu vya kufuatilia malengo 17 ya ajenda hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya Taifa ya takwimu nchini Tanzania Dkt. Albina Chuwa amesema mara baada ya kupitishwa kwa ajenda hiyo, waliitisha kikao cha wadau wanaozalisha na kutumia takwimu ili kuelezea mwelekeo unaotakiwa na sasa..
Na kuhusu takwimu na mabadiliko ya tabianchi kwa mujibu wa ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa iliyowasilishwa kwenye mkutano huo Dokta


http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/2016/03/tanzania-yajinasibu-kuhusu-takwimu-kwenye-ajenda-2030/#.VuWuIlKbkdU

TFF YAMALIZA MKUTANO WAKE MKUU SALAMA JIJINI TANGA

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) jana limefanya Mkutano Mkuu wa Mwaka katika Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga ambapo mgeni Rasmi alikua ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza.Katika hotuba yake kwa wajumbe wa mkutano huo, Mahiza aliushukuru uongozi wa TFF nchini kwa kuweza kuandaa mkutano mkuu mzuri na wa kisasa ambao pia ulifanyikia katika mkoa wake wa Tanga.
Akiongea na Wajumbe wa Mkutano Mkuu, Mahiza alisema TFF ina changamoto ambazo inapaswa kuzifanyia kazi na hasa katika kuendeleza soka la wanawake nchini ambalo mwamko wake bado uko chini.
Mahiza alisema, Mpira wa miguu kwa sasa ni ajira nzuri ambayo inasaidia kujikwamua kiuchumi kwa wachezaji pamoja na familia zao, na kuyaomba makampuni yajitokeze kuwekeza katika mpira wa miguu na hasa katika soka la wanawake.
“Mahitaji ya wanawake katika kushiriki/kucheza mpira wa miguu ni makubwa zaidi, tofauti na wanaume hivyo kuangalia jinsi gani wadhamini wanapatikana ili kuweza kuwasaidia wanawake” alisema Mahiza.
Mkutano ulijadili Ajenda za kawaida ambazo ni Kufungua Mkutano ni Uhakiki wa Wajumbe, Kuthibitisha Muhtsari wa Mkutano Mkuu uliopita, Yatokanayo na Mkutano uliopita, Hotuba ya Rais, Taarifa kutoka kwa Wanachama, Kuthibitisha ripoti ya utekelezaji wa Kamati ya Utendaji.

Zingine ni Kuthibitisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu 2013, Kuthibitisha ripoti ya Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu, Kupitisha bajeti ya 2015, Marekebisho ya Katiba, Mengineyo na Kufunga Mkutano.
Baada ya majadiliano ya kina mkutano mkuu pia uliazimia kuahirisha ajenda ya marekebisho ya Katiba hadi Mkutano Mkuu ujao utakaofanyika mwezi Disemba mwaka huuu.


Wakati huo huo Leo Jumapili asubuhi Mkuu wa Mkoa Tanga, Mwantumu Mahiza ameweka jiwe la msingi katika eneo la kituo cha michezo cha kukuzia vipaji lilipo eneo la Mikanjuni jijini Tanga.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa uwekaji jiwe la msingi, Mahiza alisema wamejisikia faraja mkoa wa Tanga kupata nafasi hiyo kuwa mkoa wa kwanza kupata kituo cha kukuzia vipaji nchini.
Mahiza alisema uongozi wa Serikali mkoa wa Tanga utashirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tanga (TRFA)/TFF katika kusaidia usimamizi wa uendeshaji wa kituo hicho.
Mahiza ameishukuru TFF kwa kuamua kuwekeza katika ujezi wa kituo hicho, ambacho baaade kitatoa nafasi kwa vijana kupata ajira kupitia mpira na shughuli nyingine za maendeleo ya kiuchumi ikiwemo utalii na watu kupata ajira katika kituo hicho.

http://tff.or.tz/news/372-tff-yamaliza-mkutano-wake-mkuu-salama-jijini-tanga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.
Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.
Wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
 1. Mh. Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
 2. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga - Mkuu wa Mkoa wa Geita.
 3. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu - Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
 4. Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga - Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
 5. Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga - Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
 6. Mh. Godfrey Zambi - Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
 7. Dkt. Steven Kebwe - Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
 8. Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven - Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
 9. Mh. Anna Malecela Kilango - Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
 10. 10.  Mhandisi Methew Mtigumwe - Mkuu wa Mkoa wa Singida.
 11. 11.  Mh. Antony Mataka - Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
 12. 12.  Mh. Aggrey Mwanri - Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
 13. 13.  Mh. Martine Shigela - Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
14. Mh. Jordan Mungire Rugimbana - Mkuu wa Mkoa Dodoma.
15. Mh. Said Meck Sadick - Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
16. Mh. Magesa Mulongo - Mkuu wa Mkoa Mara.
17. Mh. Amos Gabriel Makalla - Mkuu wa Mkoa Mbeya.
18. Mh. John Vianey Mongella - Mkuu wa Mkoa Mwanza.
19. Mh. Daudi Felix Ntibenda - Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
20. Mh. Amina Juma Masenza - Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
21. Mh. Joel Nkaya Bendera - Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
22. Mh. Halima Omary Dendegu - Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
23. Dkt. Rehema Nchimbi - Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
24. Mhandisi Evarist Ndikilo - Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
25. Mh. Said Thabit Mwambungu - Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
26. Luteni Mstaafu Chiku Galawa - Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).

Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa, wataapishwa Jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa 3:30 Asubuhi Ikulu, Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
13 Machi, 2016

http://www.ikulu.go.tz/index.php/media/news_details/2399
Picha   http://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2016/02/19/160219170013_john_magufuli_tanzania_640x360_statehousetanzania.jpg

SERIKALI YAANZA KUKUSANYA HELA KWA AJILI YA UNUNUZI WA MELI- ZIWA VICTORIAWaziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amesema Serikali imeanza kukusanya fedha kwa ajili ya kununua meli mpya kwa ajili ya usafirishaji wa abiria na mizigo kwenye Ziwa Victoria.
Waziri Mkuu MAJALIWA ametoa taarifa hiyo Mkoani KAGERA baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo ambako amewasili leo kwa ziara ya siku tatu kwa ajili ya kukagua masuala ya wakimbizi pamoja na mwenendo wa ranchi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Mbali ya ununuzi wa meli hiyo Waziri Mkuu MAJALIWA amesema Serikali pia imejipanga kununua ndege mbili ili kuimarisha usafiri wa anga hapa nchini.
Amesema suala hilo limeshafika mbali na utekelezaji wake hautachukua muda mrefu kuanzia sasa.
Alitumia fursa hiyo kuwaarifu wana Kagera kwamba hivi karibuni Serikali itaanza mradi wa kujenga bomba la kusafirisha mafuta ambalo litapita kwenye mkoa huo na hivyo kutoa ajira kwa wakazi wake.

https://web.facebook.com/tbconetanzania/ 

Friday, March 11, 2016

Mkutano Mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)tar 12-13 March 2016 jijini Tanga

Mkutano Mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliokuwa ufanyike mwezi Disemba mwaka jana sasa utafanyika wikiendi hii Jumamosi na Jumapili tar 12-13 March 2016 jijini Tanga.
Ajenda za mkutano huu ni kwa mujibu wa katiba ya TFF. Mkutano mkuu utahitimishwa kwa uwekaji wa jiwe la msingi la kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji vya uchezaji mpira, kituo kitakachojengwa jijini Tanga.
Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa hoteli ya Regal Naivera.


Chanzo:http://tff.or.tz/news/370-mkutano-mkuu-tff-machi-12-13-jijini-tanga

Juhudi Za Kurejesha Takribani Wafungwa elfu Tatu Nchini Zaendelea

Wakenya wanaotumikia vifungo gerezani katika mataifa ya kigeni wanatarajiwa kurejeshwa hapa nchini kukamilisha vifungo vyao iwapo kutakuwa na maafikiano kati ya Kenya na nchi ambao wakenya wamefungwa gerezani. Hii ni baada ya kuratibiwa kwa rasimu ya mkataba wa maelewano kuhusu kuhamishwa kwa wafungwa wa Kenya. Rasimu hiyo ya mkataba inaratibiwa na afisi ya mkuu wa sheria chini ya uongozi wa mwanasheria mkuu, Prof Githu Muigai. Stakabadhi hiyo itabuni msingi wa utekelezaji wa sheria ya kuwahamisha wafungwa ya mwaka 2015 iliyoanza kutekelezwa tarehe-12 mwezi Oktoba mwaka 2015. Pindi mikakati ya kisheria itakapobuniwa, Wakenya wanaotumikia vifungo katika mataifa ya kigeni watarejeshwa hapa nchini kukamilisha vifungo hivyo. Mkataba huo pia unatarajiwa kuratibisha matakwa ya kubadilishana wafungwa. Inakadiriwa kuwa wakenya elfu-3 wanatumikia vifungo katika mataifa ya kigeni huku magereza ya humu nchini pia yakiwa na idadi sawia ya wafungwa wa kigeni.
Juhudi Za Kurejesha Takribani Wafungwa elfu Tatu Nchini Zaendelea 
Chanzo:http://radiotaifa.co.ke/index.php/juhudi-za-kurejesha-takribani-wafungwa-elfu-tatu-nchini-zaendelea/

Rais MAGUFULI aagiza BOT kusitisha malipo ya Bil 925.9Rais Dkt. JOHN MAGUFULI ameiagiza Benki kuu ya Tanzania BOT, kusitisha malipo ya shilingi Bilioni 925.6 ambayo tayari yalishaidhinishwa na badala yake yarejeshwe Wizara ya fedha na Mipango kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki.
Rais Dokta MAGUFULI ametoa agizo hilo, katika ziara yake ya kushtukiza katika BOT, na kuzungumza na watendaji wakuu wa Benki hiyo waliojumuisha Gavana, Naibu Magavana, Wakurugenzi na Mameneja.Wakati huo huo, Rais Dkt. JOHN MAGUFULI amemuagiza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. BENO NDULU, kupitia upya orodha ya wafanyakazi wa Benki hiyo, na kuwaondoa mara moja wale wote ambao hawana ulazima wa kuwa wafanyakazi katika benki hiyo.

Chanzo: https://web.facebook.com/tbconetanzania/?fref=nf

Thursday, March 10, 2016

Fursa za mafunzo zalenga kuwainua wanawake-Tanzania

Lengo la tano la malengo ya maendeleo endelevu au Ajenda 2030 linaangazia usawa wa kijinsia. Katika kufanikisha lengo hili mikakati muhimu inapaswa kuwekwa ili kuhakikisha kwamba nchi zinafanikiwa. Moja ya mikakati muhimu katika kufanikisha lengo ni kutoa mafunzo kwa wanawake n wanaume ambako nchini Tanzania baadhi ya wanawake wamepata mafunzo yanayolenga kuwainua kiuchumi. Benson Mwakalinga kutoka Redio Washirika Kyela FM ya Mbeya Tanzania amezungumza na baadhi yao, ungana naye katika makala hii Wanawake nchini Tanzania.(Picha:UN Photo/ B Wolff


.http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/2016/03/fursa-za-mafunzo-zalenga-kuwainua-wanawake/#.VuJguFKbkdU

Kasi ya kudhibiti madawa ya kulevya iendane na matibabu kwa waathirika- Ripoti INCB

Ripoti mpya ya Bodi ya kimataifa ya kuzuia madawa ya kulevya, INCB, imeshauri serikali duniani kuhakikisha harakati za kudhibiti upatikanajiwa dawa za kulevya zinaenda sambamba na harakati za kuwapatia dawa za matibabu waathirika wa madawa hayo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa riptoi hiyo nchini Tanzania Afisa mradi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya udhibiti wa madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC nchini humo Immaculate Malyamkono amesema
(Sauti ya Immaculate)
Mapema Mkuu wa kitengo cha elimu, habari na takwimu kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti dawa za kulevya nchini Tanzania Dkt. Amani Msami amezungumzia hali ya huduma za matibabu nchini Tanzania.

 Uzinduzi ripoti mpya ya Bodi ya kimataifa ya kuzuia madawa ya kulevya, INCB.(Picha:UNIC/Tanzania)

Dokta JOHN MAGUFULI amesisitiza umuhimu wa TANZANIA kujifunza mbinu mbalimbali kutoka VIETNAM

Tanzania na Vietnam zakubaliana kushirikiana katika sekta mbalimbali
TANZANIA na VIETNAM zimekubaliana kushirikiana katika nyanja za mawasiliano, elimu, kilimo, biashara na uvuvi ili kukuza uchumi wa nchi zote mbili ambazo zina mahusiano kwa takribani Miaka HAMSINI sasa.
Hayo yamebainishwa na viongozi wa nchi hizo Rais JOHN MAGUFULI pamoja na Rais TROUNG TANG SAN wa VIETNAM wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa kwa ajili ya Rais huyo wa VIETNAM Ikulu Jijini DSM.
Akizungumza katika dhifa hiyo Dokta JOHN MAGUFULI amesisitiza umuhimu wa TANZANIA kujifunza mbinu mbalimbali kutoka VIETNAM ambazo nchi hiyo ilizitumia na kuweza kukuza uchumi wake.
Kwa upande wake Rais TRUONG TANG SAN ambaye anafanya ziara ya kwanza Barani Afrika huku akiwa rais wa pili wa nchi hiyo kuzuru TANZANIA tangu mwazoni mwa Miaka ya SABINI amesisitiza kuwa uhusiano uliojengwa na waasisi wa mataifa haya mawili lazima uenziwe na kulindwa kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili..


https://web.facebook.com/tbconetanzania/