VICHWA VYA HABARI

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks t>

Sunday, March 13, 2016

Nyumba za chama cha CCM zachomwa Pemba, Zanzibar

Watu wasiojulikana wamechoma moto nyumba za Chama Cha Mapinduzi kisiwani Pemba huku duru ya pili ya uchaguzi ikitarajiwa Machi 20.
Kamishena wa polisi wa eneo la Pemba Kusini Mohamed Shakani amesema watu hao wamechoma maeneo 11 ya kufanyia mikutano na zahanati moja lakini hakuna aliyejeruhiwa.
Amesema mshukiwa mmoja kwa jina Mohamed Ramadhan Seif amekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Shakani anasema uchunguzi wa mwanzo umeonyesha kuwa waliotekeleza kitendo hicho walinyunyiza petroli kwenye nyumba hizo katika barabara ya Kibirizi pamoja na maeneo ya mikutano ya Kiwani na Mwambe na kuwasha moto.
Waziri kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais Mohamed Aboud Mohamed amezuru maeneo hayo na kuwataka raia kusaidia kuwatambua waliotekeleza uchomaji huo.

http://swahili.cri.cn/141/2016/03/13/1s151664.htm 

0 comments:

Post a Comment