VICHWA VYA HABARI

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks t>

Friday, April 22, 2016

Uganda mwenyeji wa mkutano kuhusu miundombinu


ICGLR, Kampala, Agosti 7, 2012.
REUTERS/Edward Echwalu

    
 
Marais wa Kenya, Uganda, Rwanda na Sudan Kusini wanatarajiwa kukutana kesho jijini Kampala nchini Uganda katika kikao cha 13 kujadili kuhusu maendeleo ya miundo mbinu zinazounganisha nchi hizo nne.







Miongoni mwa miradi ambayo mataifa hayo yanashirikiana ni pamojana ujenzi wa reli ya Kati na ujenzi wa bomba la kusafiria mafuta.
Inaelezwa kuwa, Uganda inatarajiwa kufafanulia Kenya kwenye kikao hicho ni kwanini umeamua kujenga bomba lake la kusafirishia kupitia bandari ya Tanga.
Hayo yakijiri, viongozi wa Kenya, Uganda na Tanzania mwishoni mwa wiki wanatarajiwa kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda na Kenya hadi pwani.
Mwaka jana, Kenya na Uganda zilikuwa zinashauriana kuhusu mpango wa kujenga bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima, magharibi mwa Uganda, hadi bandari ya Lamu katika Pwani ya Kenya.
Bomba hilo la mafuta lilikusudiwa kutumiwa kusafirisha mafuta ghafi kutoka eneo la Ziwa Albert nchini Uganda na kutoka eneo lenye mafuta la Lokichar nchini Kenya.
http://www.kiswahili.rfi.fr/eac/20160422-uganda-mwenyeji-wa-mkutano-kuhusu-miundombinu


0 comments:

Post a Comment