VICHWA VYA HABARI

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks t>

Friday, April 15, 2016

Sudan Kusini yaingia rasmi Afrika MasharikiRais Kiir amesema Sudan Kusini imejiunga na jumuiya sahihi

Sudan Kusini sasa ni mwanachama mpya wa jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kusaini mkataba wa kujiunga rasmi na jumuiya hiyo.
Rais Kiir ametia saini mkataba huo jijini Dar es Salaam mbele ya mwenyeji wake Rais wa Tanzania John Magufuli ambaye kwa sasa ndiye Mwenyeketi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Amesema kujiunga kwa nchi yake na jumuiya hiyo kumemfanya kujihisi kuwa kwenye jumuiya sahihi.
“Ninaposimama hapa leo hii, moyo wangu umejawa na furaha na hali ya kuridhishwa kuwa sehemu ya jumuiya hii kuu. Kwa ujasiri kabisa ninaweza kusema hatimaye Sudan Kusini imepata mahala sahihi katika jumuiya,” alisema Rais Kiir.
Viongozi wa nchi za jumuiya hiyo waliidhinisha kukubaliwa kwa Sudan Kusini kujiunga na jumuiya hiyo kwenye mkutano mkuu uliofanyika mjini Arusha mwezi uliopita.
Sudan Kusini ndiyo nchi ya sita kujiunga na jumuiya hiyo iliyoanza kwa nchi tatu Tanzania, Kenya na Uganda. Rwanda na Burundi zilijiunga na jumuiya hiyo baadaye.
Sudan Kusini sasa inatarajiwa kufungua mipaka yake kwa ajili ya biashara. Tayari kampuni na asasi nyingi za kifedha kutoka Kenya zimefungua biashara nchini Sudan Kusini.
Wengi wanatarajia hatua ya leo itafungua fursa zaidi za kibiashara kati ya Sudan Kusini na nchi wanachama wa jumuiya.
Wadadisi wengine wanaamini kuwa baadhi ya miradi ambayo Sudan Kusini ingetaka kujumuishwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni miundo msingi ikiwemo reli na mabomba ya mafuta.
http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/04/160415_southsudan_new_eac 

0 comments:

Post a Comment