VICHWA VYA HABARI

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks t>

Tuesday, April 19, 2016

Daresalaam Tanzania:Wananchi kuwezehswa kiuchumi

Katoro FM (File)
Baraza la Taifa la Tanzania la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) limewataka waratibu wa uwezeshaji katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, kutumia mafunzo waliyopata kulisaidia baraza hilo kufikia malengo yake ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Beng'i Issa amesema waratibu hao wana wajibu wa kuhakikisha wanatumia ujuzi walioupata kwa faida ya wananchi katika mikoa yao.
Jumla ya waratibu 41 wa madawati ya uwezeshaji kutoka katika mikoa ya Ruvuma, Iringa, Njombe, Rukwa, Songwe na Mbeya walipatiwa mafunzo ya siku tatu jijini Mbeya.
Mafunzo hayo yalimalizika mwishoni mwa wiki na waliopewa mafunzo wametakiwa kufanya kazi kwa niaba ya baraza kutekeleza sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Alisema mafunzo hayo yamelenga kuwapatia ufahamu wa kujua wajibu wao, kufanya kazi na jamii, kuibua fursa, kuwaonyesha fursa wananchi na kuwaunganisha na vyombo vya fedha na mifuko ya serikali kupata mikopo kuendeleza shughuli za kijasiriamali.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa NEEC, mafanikio na changamoto zitakazojitokeza katika kanda hiyo zitatumika katika kuboresha kanda nyingine zilizobaki.

http://swahili.cri.cn/141/2016/04/19/1s152677.htm

0 comments:

Post a Comment