Serikali ya Tanzania imesema itaanza kutekeleza ahadi ya rais John
Magufuli ya kukipa kila kijiji nchini Shilingi milioni 50 katika mwaka
wa fedha wa 2016-2017.
Akizungumza bungeni, naibu waziri ofisi ya rais, Bw Antony Mavunde
amesema utaratibu wa kugawa fedha hizo unaandaliwa na baraza la
uwezeshaji wananchi kwa kushirikiana na wizara ya Utawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa.Ameongeza kuwa vigezo ambavyo vimekuwa vikitumika
katika kutoa mikopo na mitaji kwa vijana ni umri usiozidi miaka 35
ambapo vijana watahitajika kujiunga na Saccos za wilaya na kuunda
vikundi na kuvisajili kisheria.Amesema ili kuhakikisha vijana wanakuwa
wajasiriamali na wanaweza kupatiwa mikopo na mitaji, serikali imejiwekea
mikakati ya kutambua vijana na mahitji yao katika ngazi mbalimbali na
kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi mbalimbali ya vijana.
http://swahili.cri.cn/141/2016/04/22/1s152772.htm
file katoro fm |
http://swahili.cri.cn/141/2016/04/22/1s152772.htm
0 comments:
Post a Comment