Picha File Katoro Fm |
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego alisema mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa kuwasili kwa wawekezaji hao ni fursa ya pekee kwa mkoa huo.
Alisema wafanyabiashara hao wamelenga kuwekeza katika maeneo mbalimbali ikiwamo sekta za kilimo, utalii, gesi na mafuta.
Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asili Madimba, Mhandisi Nkilila Lucas alisema wafanyabiashara hao wana jukumu la kuwekeza katika sekta ya mafuta na gesi.
Mfanyabiashara kutoka Oman, Mansul Hemed alisema ziara hiyo imelenga kuangalia shughuli za uwekezaji na jinsi watakavyoweza kutoa elimu.
Alisema wafanyabiashara wa Kitanzania kwa sasa wanaweza kupeleka bidhaa zao Oman kama vile mifugo na mazao yanayolimwa nchini.
Wafanyabiashara hao wamewasili nchini na kutembelea maeneo mbalimbali yenye fursa za kiuchumi
http://swahili.cri.cn/141/2016/04/20/1s152718.htm
0 comments:
Post a Comment