VICHWA VYA HABARI

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks t>

Sunday, April 17, 2016

Tanzania yaweka mipango ya kupunguza msongamano wa magari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DK.Magufuli(file)
Rais John Magufuli wa Tanzania ametangaza mipango ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.
Amesema baadhi ya mipango hiyo ni pampja na kuwekeza ujenzi wa barabara na reli katika mji huo wenye wakaazi milioni tano.
Rais Magufuli aliyasema hayo wakati akizindua ujenzi wa barabara ya juu jijini humo.
Amesema barabara ya kilomita 128 yenye laini sita itajengwa kutoka Kigamboni Bridge hadi eneo la pwani la Chalinze ikiwa na madaraja matano ya juu.
Rais Magufuli pia amesema tayari serikali imetenga dola milioni 500 kwenye mwaka ujao wa fedha kufanyia ukarabati reli ya mjini ili iwe ya kisasa.

0 comments:

Post a Comment