VICHWA VYA HABARI

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks t>

Sunday, April 17, 2016

Annan: Nkurunziza hakustahili kuwania urais

Rais Nkurunziza
Aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa bwana Kofi Annan amemkosoa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kwa kuwania muhula wa tatu.
Bw Annan amesema Nkurunziza anafahamu vyema kuwa ni kinyume cha katiba ya taifa hilo kuwania madaraka kwa zaidi ya vipindi viwili.

Raia huyo wa Ghana anamlaumu rais Nkurunziza kwa kusababisha maandamano yaliyosababisha vifo vya takriban watu mia nne.
Bw Annan ameiambia BBC kuwa bw Nkurunziza haoneshi dalili zozote za kutafuta suluhu la amani wala nia ya kutaka mazungumzo ya kweli na wapinzani wake.
Bw Annan ameiambia BBC kuwa bw Nkurunziza haoneshi dalili zozote za kutafuta suluhu la amani.

Katibu huyo wa zamani ameiomba jamii ya imataifa kuyasaidia mataifa ya Afrika yanayokabiliwa na matatizo chungu nzima kama vile Ethiopia inayokabiliwa na baa la njaa
Annan anasema kuwa mataifa hayo ya Afrika yamesahaulika huku kurunzi ya ulimwengu ikiangazia Syria na mataifa ya Mashariki ya kati http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/04/160417_annan_on_burundi

0 comments:

Post a Comment