VICHWA VYA HABARI

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks t>

Thursday, March 17, 2016

Vijana wandelea kutowakilishwa katika mabunge duniani : Ripoti

Nembo ya IPU.(Picha@IPU)
Ripoti mpya ya muungano wa mabunge duniani IPU inaonyesha kuendelea kwa tatizo sugu la kutowakilishwa ipasavyo kwa vijana katika mabunge, wakati huu ambapo idadi ya kundi hilo duniani ni ikubwa kuliko wakati wowote ule.
Ripoti hiyo iitwayo uwakilishi wa vijana katika mabunge ya kitaifa 2016, iliyozinduliwa leo wakati wa mkutano kuhusu wabunge vijana unaofanyika mjini Lusaka Zambia, imeabaini kwamba ni asilimia 1.9 pekee kati ya wabunge 45,000 wana umri chini ya miaka 30.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa hakuan ongezeko kutokana na utafiti wa IPU wa mwaka 2014 ambapo pia ripoti imeonyesha kuwa karibu theluthi ya mabunge madogo na karibuasilimai 80 ya mabaraza ya seneti hayana hata mbunge mmoja mwenye umri wa chini ya miaka 30.
Hata hivyo ripoti mpya hiyo imetaja nchi ambazo zimepiga hatua katika kuwajumisha vijana katika mabunge yao kuwa ni Sweden, Ecuador, Finland na Norway ambazo zina asilimia 10 au zaidi ya wabunge wenye umri wa chiniya miaka 30.
Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mjumbe wa vijana katika Umoja wa Mataifa, Ahmad Alhendawi, amesema kuna haja ya kutafuta njia za kuwashirikisha vijana zaidi, hata kutumia teknohama.
(Sauti ya Alhendawi)
"Ningependa kusisitiza umihimu wa kutambua kuwa vijana wanataka kushiriki na wana uwezo wa kushiriki, na tusiwalaumu tu bila kujua ni kwa nini hawashiriki, kwa sababu wakati mwingine kuna vizuizi vikubwa vya kimfumo."

http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/2016/03/vijana-wandelea-kutowakilishwa-katika-mabunge-duniani-ripoti/#.VurnflKbkdU 

0 comments:

Post a Comment