Kator fm (File)
Viongozi wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki wametangaza kuwa bomba la mafuta la Uganda kutoka Hoima hadi
Bandari ya Tanga litapitia Tanzania, mradi ambao unatarajiwa kugharimu
dola za kimarekani bilioni 4.
Viongozi hao wamefanya uamuzi huo kwenye Mkutano...
Sunday, April 24, 2016
Nguli wa muziki wa Rhumba, Papa Wemba afariki dunia

Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba,
anaejulikana kwa jina maarufu Papa Wemba, ameiaga dunia akiwa katika
jukwaa Jumapili Aprili 24. Mwanamuziki huyu nguli wa Congo (DRC)
alikuwa na udhaifu wakati wa tamasha aliloendesha nchini Cote d'Ivoire
Jumamosi Aprili 23.http://www.kiswahili.rfi.fr/utamaduni/20160424-gwiji-wa-muziki-wa-kiafrika-papa-wemba-afariki
Papa...
Friday, April 22, 2016
Uganda mwenyeji wa mkutano kuhusu miundombinu
ICGLR, Kampala, Agosti 7, 2012.REUTERS/Edward Echwalu
Marais wa Kenya, Uganda, Rwanda na Sudan Kusini wanatarajiwa kukutana kesho jijini Kampala nchini Uganda katika kikao cha 13 kujadili kuhusu maendeleo ya miundo mbinu zinazounganisha nchi...
Serikali ya Tanzania ndio mmiliki wa kampuni ya General Tyres Arusha

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, wa Tanzania Bw Charles Mwijage
amesema hivi sasa kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre
Arusha kinamilikiwa na serikali baada ya serikali kununua asimilia 26
kutoka kwa mbia wake. Akizungumza bungeni, Bw Mwijage amesema...
Ukuaji wa sekta ya viwanda bado uko nyuma Tanzania

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya bajeti nchini Tanzania imesema ukuaji wa
sekta ya viwanda katika awamu ya kwanza ya mpango wa maendeleo ya taifa
ulikuwa chini ya lengo, jambo ambalo haliridhishi maendeleo ya uchumi wa
viwanda.
Akizungumza na radio China kimataifa, mwenyekiti...
Tanzania kuanza kutekeleza ahadi ya Magufuli

Serikali ya Tanzania imesema itaanza kutekeleza ahadi ya rais John
Magufuli ya kukipa kila kijiji nchini Shilingi milioni 50 katika mwaka
wa fedha wa 2016-2017.
file katoro fm
Akizungumza bungeni, naibu waziri ofisi ya rais, Bw Antony Mavunde
amesema utaratibu wa kugawa...
Wednesday, April 20, 2016
Wafanyabiashara 13 kutoka nchini Oman wawasili mkoani Mtwara nchini Tanzania kuangalia fursa za uwekezaji

Picha File Katoro Fm
Wafanyabiashara 13 kutoka nchini Oman wamewasili mkoani Mtwara nchini
Tanzania kuangalia fursa za uwekezaji na jinsi watakavyoshirikiana na
Watanzania katika masuala ya kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego alisema mwishoni mwa wiki
iliyopita...
Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania atoa onyo la ugonjwa wa mnyauko katika mikorosho kwa wakulima

Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Mfaume Juma(file Katoro fm)
Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Mfaume Juma amesema
kuingia kwa ugonjwa wa mnyauko katika mikorosho ni tishio katika zao
hilo na kuwapa hofu wakulima.
Akizungumza na waandishi wa...
Tuesday, April 19, 2016
Mfugaji wa Tanzania ashinda tuzo ya kimataifa ya mazingira

Bw Edward Loure.mshindi wa tuzo ya
mazingira ya Goldman kwa mwaka huu
Mfugaji wa kabila la wamaasai kutoka Tanzania ameshinda tuzo ya
mazingira ya Goldman kwa mwaka huu, kutokana na njia yake ya kipekee ya
kulinda mazingira na jamii yake kwa ujumla.
Tuzo hii inatolewa...
Daresalaam Tanzania:Wananchi kuwezehswa kiuchumi

Katoro FM (File)
Baraza la Taifa la Tanzania la
Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) limewataka waratibu wa uwezeshaji
katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, kutumia mafunzo waliyopata
kulisaidia baraza hilo kufikia malengo yake ya kuwawezesha wananchi
kiuchumi.
Katibu...
Mugabe alalamikia askofu kuhusu ndoa za jinsia moja

Rais Mugabe hupinga sana wapenzi wa jinsia moja
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alikutana na Askofu mkuu wa Canterbury na kuibua maswali kuhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Askofu
mkuu Justin Welby amesema alimjibu kiongozi huyo kwamba kuna mitazamo
tofauti kuhusu ndoa...
DARAJA LA KIGAMBONI SASA NI DARAJA LA MWL. NYERERE

Rais Magufuli ametoa tamko hilo kwa Waziri wa Ujenzi, kulipa jina la Nyerere ikiwa ni kuenzi kazi kubwa aliyoifanya baba wa taifa ya kuwaunginisha watanzania.
Hayo ameyasema muda si mrefu katika uzinduzi wa daraja hilo maarufu kama Daraja la Kigamboni. Daraja ambalo ni...
Monday, April 18, 2016
Daraja la kisasa kuzinduliwa Kigamboni

File
Rais Joseph Pombe Magufuli wa Tanzania atafungua daraja la Kigamboni hapo kesho.
Daraja hilo litaunganisha eneo la Kigamboni na mji wa Dar es Salaam.
Ujenzi wa daraja hilo umegharimu zaidi dola milioni 140.
Daraja la Kigamboni linatarajiwa kurahisisha usafiri na...
Tanzania: Bajeti ya Afya imeongezwa Hadi 250bn Kutoka 41bn

.Bi
Ummy Mwalimu (Katoro Fm File)
Serikali ya Tanzania imeongeza bajeti yake kwa ajili ya ununuzi wa dawa
kutoka sh bilioni 41 katika mwaka wa fedha wa 2014/15 hadi sh bilioni
251 katika mwaka wa 2015/16 kushughulikia uhaba wa dawa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,...
Sunday, April 17, 2016
Watoto Geita walazimika kuchagua kati ya chakula na masomo
Ingawa serikali ya Tanzania inataka kutoa elimu kwa kila mtoto, baadhi
ya watoto wa mkoani Geita wamesema wanapendelea kufanya kazi migodini au
kuvua samaki kwani familia zao hazina pesa ya kutosha na hawataki
kulala njaa. Hawa Bihoga amewatembelea na kushuhudia hali ya maisha yao.
fuatilia link kwa habari zaidihttp://www.dw.com/sw/watoto-geita-walazimika-kuchagua-kati-ya-chakula-na-masomo/av-19183127...
Annan: Nkurunziza hakustahili kuwania urais

Rais Nkurunziza
Aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa
mataifa bwana Kofi Annan amemkosoa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kwa
kuwania muhula wa tatu.
Bw Annan amesema Nkurunziza anafahamu
vyema kuwa ni kinyume cha katiba ya taifa hilo kuwania madaraka kwa
zaidi ya vipindi...
Filamu nyingine ya Avatar kuongezwa

Watengenezaji wa filamu ya Avatar
franchise wamesema kutatolewa filamu zaidi katika mwendelezo huo wa
filamu, filamu ijayo ikitarajiwa kutolewa 2018.
Mwelekezi wa filamu hizo James Cameron ametangaza kwamba filamu hizo zitaendelezwa hadi makala ya tano itakayotolewa...
Tanzania yaweka mipango ya kupunguza msongamano wa magari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DK.Magufuli(file)
Rais John Magufuli wa Tanzania ametangaza mipango ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.
Amesema baadhi ya mipango hiyo ni pampja na kuwekeza ujenzi wa barabara na reli katika mji huo wenye wakaazi...
Saturday, April 16, 2016
Tanzania yaimarisha oparesheni dhidi ya bangi

Bangi(Maktaba) ktfm
Polisi nchini Tanzania wameendeleza oparesheni dhidi ya ukuzaji wa bangi
pamoja na biashara yake kwenye eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo la
Arusha.
Oparesheni hiyo inaendelezwa huku ripoti ya Umoja wa Mataifa
ikionyesha kuwa Tanzania ndio mzalishaji...
Friday, April 15, 2016
Timu 4 zatinga nusu fainali
Hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imepigwa Alhamisi hii, Aprili 14 kwa michezo min...
Wawekezaji wa madini Tanzania wataka kujadili na serikali yao jinsi ya kuboresha mazingira ya biashara hiyo

kutoka mataba katoro fm
madini hali ambayo itawatorosha wawekezaji wa kigeni.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya maofisa wa migodi ya madini
nchini humo wamesema kuna changamoto kadhaa ambazo zimechangia
wawekezaji katika sekta ya madini kutowekeza kwenye utafutaji...
Sudan Kusini yaingia rasmi Afrika Mashariki

Rais Kiir amesema Sudan Kusini imejiunga na jumuiya sahihi
Sudan Kusini sasa
ni mwanachama mpya wa jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya Rais wa nchi
hiyo Salva Kiir kusaini mkataba wa kujiunga rasmi na jumuiya hiyo.
Rais
Kiir ametia...
Rais wa Tanzania John Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw Gabriel Nderumaki.

Dkt Magufuli amemteua Bi Abdallah kuwa kaimu
Bi Tuma Abdallah, ambaye amekuwa mhariri mtendaji msaidizi wa magazeti ya serikali (TSN), ameteuliwa kuwa kaimu.
Hakuna maelezo yoyote zaidi yaliyotolewa kuhusu sababu za kutenguliwa kwa uteuzi wa Bw Nderumaki.
TSN huchapisha...