Waziri Mkuu Aagiza OR TAMISEMI Kusimamia Mikoa na Halmashauri Kuleta Maendeleo tarajiwa |
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Kassim Majaliwa Majaliwa ameitaka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa-(OR-TAMISEMI) kuhakikisha inaisimamia vizuri Mikoa na
Halmashauri ili serikali iweze kupata matokeo mazuri na
tarajiwa.Akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI
alipoitembelea ofisi ya TAMISEMI mjini Dodoma leo, Mhe. Waziri Mkuu
alisema jukumu kubwa lililopo hivi sasa katika Mamlaka za Serikali za
Mitaa ni kuhakikisha kuwa zinabuni vyanzo vipya vya mapato na kusimamia
vizuri ukusanyaji wa mapato ya serikali.
“Hatukubaliani
na uzembe kwenye idara na halmashauri za wilaya kwakuwa hivi sasa
serikali ya awamu ya tano inasimamia utumishi wa uadilifu hivyo kila
mmoja ahakikishe anasimamia vizuri eneo lake†alisema Mhe.
MajaliwaAlisema serikali ya awamu ya tano imekusudia kuwahudumia
ipasavyo watanzania wenye uelewa tofauti na matakwa tofauti na kwa
kuanzia serikali imeanza kuwajenga watumishi wa serikali kutambua na
kukumbuka kuwa wao ni wahudumu wa wananchi hivyo inawapasa kuwahudumia
vema.
“Lazima tujenge moyo wa huruma wa
kuwahudumia wenzetu, anapokuja mwananchi msikilize, muhudumie na
mwelekeze eneo sahihi ili aweze kupata huduma. Lazima tusimamie na
kuona maeneo yote yanafanya kazi kama ilivyokusudiwa, ili kupata matokeo
tarajiwa iwe ni wajibu ya kila mmoja kuhakikisha kuwa anatoa usimamizi
thabiti katika eneo lake.†alisisitiza Mhe. Waziri Mkuu.
Akimkaribisha
Mhe. Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George
Simbachawene alisema TAMISEMI wapo tayari kubadilika na kufanya kazi
kama kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe
Magufuli –HAPA KAZI TU-.
http://www.pmoralg.go.tz/newseventsinfo/habari-1100-20160121-Waziri-Mkuu-Aagiza-OR-TAMISEMI-Kusimamia-Mikoa-na-Halmashauri-Kuleta-Maendeleo-tarajiwa/
http://www.pmoralg.go.tz/newseventsinfo/habari-1100-20160121-Waziri-Mkuu-Aagiza-OR-TAMISEMI-Kusimamia-Mikoa-na-Halmashauri-Kuleta-Maendeleo-tarajiwa/
0 comments:
Post a Comment