Wakenya wanaotumikia vifungo gerezani katika mataifa ya kigeni
wanatarajiwa kurejeshwa hapa nchini kukamilisha vifungo vyao iwapo
kutakuwa na maafikiano kati ya Kenya na nchi ambao wakenya wamefungwa
gerezani. Hii ni baada ya kuratibiwa kwa rasimu ya mkataba wa maelewano
kuhusu kuhamishwa kwa wafungwa wa Kenya. Rasimu hiyo ya mkataba
inaratibiwa na afisi ya mkuu wa sheria chini ya uongozi wa mwanasheria
mkuu, Prof Githu Muigai. Stakabadhi hiyo itabuni msingi wa utekelezaji
wa sheria ya kuwahamisha wafungwa ya mwaka 2015 iliyoanza kutekelezwa
tarehe-12 mwezi Oktoba mwaka 2015. Pindi mikakati ya kisheria
itakapobuniwa, Wakenya wanaotumikia vifungo katika mataifa ya kigeni
watarejeshwa hapa nchini kukamilisha vifungo hivyo. Mkataba huo pia
unatarajiwa kuratibisha matakwa ya kubadilishana wafungwa. Inakadiriwa
kuwa wakenya elfu-3 wanatumikia vifungo katika mataifa ya kigeni huku
magereza ya humu nchini pia yakiwa na idadi sawia ya wafungwa wa kigeni.
Juhudi Za Kurejesha Takribani Wafungwa elfu Tatu Nchini Zaendelea
Chanzo:http://radiotaifa.co.ke/index.php/juhudi-za-kurejesha-takribani-wafungwa-elfu-tatu-nchini-zaendelea/
0 comments:
Post a Comment