VICHWA VYA HABARI

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks t>

Sunday, March 13, 2016

SERIKALI YAANZA KUKUSANYA HELA KWA AJILI YA UNUNUZI WA MELI- ZIWA VICTORIAWaziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amesema Serikali imeanza kukusanya fedha kwa ajili ya kununua meli mpya kwa ajili ya usafirishaji wa abiria na mizigo kwenye Ziwa Victoria.
Waziri Mkuu MAJALIWA ametoa taarifa hiyo Mkoani KAGERA baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo ambako amewasili leo kwa ziara ya siku tatu kwa ajili ya kukagua masuala ya wakimbizi pamoja na mwenendo wa ranchi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Mbali ya ununuzi wa meli hiyo Waziri Mkuu MAJALIWA amesema Serikali pia imejipanga kununua ndege mbili ili kuimarisha usafiri wa anga hapa nchini.
Amesema suala hilo limeshafika mbali na utekelezaji wake hautachukua muda mrefu kuanzia sasa.
Alitumia fursa hiyo kuwaarifu wana Kagera kwamba hivi karibuni Serikali itaanza mradi wa kujenga bomba la kusafirisha mafuta ambalo litapita kwenye mkoa huo na hivyo kutoa ajira kwa wakazi wake.

https://web.facebook.com/tbconetanzania/ 

0 comments:

Post a Comment