VICHWA VYA HABARI

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks t>

Tuesday, March 15, 2016

Rais Magufuli asema hasara ya mishahara hewa inafikia billioni 2.5 kwa mwezi

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli akitoa hotuba ya kitaifa
Rais wa Tanzania  John Magufuli amewaapisha wakuu wa mikoa aliowateua hivi karibuni nchini humo huku akizungumzia upotevu mkubwa wa mapato ya serikali unaotokana na kuwepo watumishi hewa
Akizungumza mara baada ya kuwaapisha wakuu hao  wa mikoa rais Magufuli amesema tatizo la wafanyakazi hewa limekuwa likigharimu serikali fedha nyingi, ambapo ametolea mfano wa uchunguzi uliofanywa katika mikoa miwili ya Dodoma na singida na kubaini takriban wafanyakazi hewa 202 katika halmashauri 14.
Amesema kutokana na hali hiyo na ikichukuliwa taswira ya nchi nzima, hasara inayokisiwa inayotokana na malipo ya mishahara hewa ya wafanyakazi nchini  Tanzania inafikia shilingi billioni 2.5 kila mwezi  huku serikali ikitumia shilingi bilioni 549 kwa mwezi kwa ajili kulipa watumishi wake hivyo amewataka kuzisimamia vyema halmashauri zao.
Wakuu wa mikoa wote 25 walioapishwa baadaye wamesaini kiapo cha uadilifu kilichosimamiwa na kamishna wa maadili ya viongozi wa umma Salome Kaganda, huku makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  akiwatahadharisha juu ya kusimamia vyema matumizi ya fedha za maendeleo.
Rais Magufuli pia  amewaapisha kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA,  Alphayo Kidata na Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa-Takukuru,  Valentine  Mlowola aliyewathibitisha kazini hivi karibuni baada ya kukaimu kwa muda nafasi hizo.

http://www.voaswahili.com/content/tanzania-mishahara-hewa-magufuli/3238329.html

0 comments:

Post a Comment