Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba,
anaejulikana kwa jina maarufu Papa Wemba, ameiaga dunia akiwa katika
jukwaa Jumapili Aprili 24. Mwanamuziki huyu nguli wa Congo (DRC)
alikuwa na udhaifu wakati wa tamasha aliloendesha nchini Cote d'Ivoire
Jumamosi Aprili 23.http://www.kiswahili.rfi.fr/utamaduni/20160424-gwiji-wa-muziki-wa-kiafrika-papa-wemba-afariki
|
Papa Wemba, mwimbaji na mtunzi wa Muziki wa Afrika.
© E. Sadaka
|
Msemaji wa serikali, Lambert Mende imeelezea huzuni ilio nao kwa kumpoteza msanii
mkuu Papa Wemba, mfalme wa muziki wa Rumba.
Nyota wa soka wa Cameroon, Samuel Eto'o, ameelezea kuwa ana huzuni mkubwa kuona amemkosa gwiji wa muziki wa Kiafrika.
Waandaaji wa tamasha la miziki ya miji ya Anoumabo (FEMUA), ndio
wametangaza kifo chake Jumapili asubuhi. Papa Wemba alikuwa na umri wa
miaka 66. Raia wa Afrika ya Kati na kungineko wamejawa na huzuni na
hisia.
Papa
Wemba alikua na udhaifu wakati wa tamasha alilopiga mjini Abidjan,
Jumamosi, Aprili 23, katika tamasha la FEMUA 2016, ikiwa ni tamasha la
miziki ya miji ya Anoumabo. Amefariki alipofikishwa hospitalini Jumapili
asubuhi, baada ya kuanguka ghafla akiwa jukwaani. Kifo chake
kimetangazwa saa sita mchana na waandaaji wa FEMUA.
Udhaifu kwenye jukwaa
Hisia kubwa na huzuni mjini Abidjan Jumapili hii, mwandishi wetu,
Olivier Rogez, amearifu. Mwanamuziki, ambaye alikua akihitimisha tamasha
hilo, alikuwa kwenye jukwaa saa 11:00 alfajiri. Kulikua na joto kubwa
na Papa Wemba alikua na ishara ya uchovu. Aliomba mara kadhaa kuongeza
sauti ya vipaza sauti. Mwanamuziki huyo nguli wa Congo alianguka
alipokua akiimba mwimbo wa nne.
Papa Wemba aliondolewa kwenye jukwaa baada ya kupoteza fahamu.
aliondolewa sehemu hiyo na timu za waokoaji, Olivier Rogez amearifu, na
kusafirishwa katika hospital ya karibu lakini mwanamuziki huyo hakuwa na
muda tena wa kuishi duniani.
"Wakati nitakua bado na uwezo wa kuimba, nitaimba,"
alisema Papa Wemba siku chache kabla ya kifo hicho kumkuta, ametoa
ushuhuda Claudy Siar akiwa mjini Abidjan, ambako pia anahudhuria tamasha
la FEMUA kwa niaba ya RFI.
Mwanamuziki nguli wa muziki wa Rumba
Papa Wemba alizaliwa mwezi Juni 1949 katika jimbo la Kasai-Masharikil
(DRC), na alikua gwiji wa muziki wa Kiafrika. Katika miaka ya 1950,
muziki wa Rumba kutoka Congo ulitawala barani Afrika na bado unatikisa
na kuchezwa jukwaa mbalimbali barani la Afrika. Papa Wemba pamoja na
bendi ya Zaiko Langa Langa waliinua Rumba kwa kiasi fulani na kweza
kuchezwa katika jukwa za kimataifa.
Wasifu wa Papa Wemba
Papa Wemba alikuwa mwanzilishi wa studio na bendi ya Viva la Musica
mwaka 1977, na alicheza nyimbo kama vile Analengo mwaka 1980, na baadaye
Maria Valencia au Yolele, nguli wa
"muziki wa dunia". Ni kwa msaada wa mwanamuziki wa Uingereza Peter Gabriel ndiye alimfanya Papa Wemba kujulikana duniani.
Papa Wemba aligundua na aliweza kuvipa mafunzo vizazi vya wanamuziki wa Afrika kama Koffi Olomide.
Papa Wemba alishiriki katika vipindi vingi vinavyorushwa hewani na RFI.